Sunday, July 21, 2013

Mourinho amrudisha Drogba darajani

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anamtaka mshambuliaji wa Galatasaray Didier Drogba arejee tena huko darajani wakimuongeza na kazi ya ukocha.

Mourinho anataka hilo lifanyike kwenye usajili huu wa majira ya joto na kama atabaniwa kuondoka na timu yake ambako amebakisha mkataba wa mwaka mmoja basi yupo tayari kusubiri mpaka mkataba huo utakapomalizika.

Chelsea wanaamini kuwa mshambuliaji huyo bado anaweza kucheza kwa kiwango cha juu kwa miaka mingine mitatu na akiwa StamfordBridge ataendelea kuwa kocha na wakitaka ajishughulishe na timu za vijana atakaporejea kwenye timu hiyo.

Drogba alikwenda kumsalimia Mourinho kwenye viwanja vya mazoezi vya Chelsea Cobham wakati wa maandalizi ya kabla ya kuanza kwa msimu.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.