Tuesday, July 23, 2013

BREAKING NEWS : Simba yatimua wachezaji wa kigeni

Sasa ni rasmi na si maneno tena,Wekundu wa Msimbazi Simba wamethibitisha kuwapiga panga wachezaji wake raia wa kigeni waliokuwa wakichezea kikosi hicho msimu uliopita na wale waliokuwa wakiwania kusajiliwa na klabu hiyo kwa msimu ujao.

Akizungumza na blog ya Supermariotz Katibu mkuu wa Simba Evodius Kajuna Mtawala amesema wachezaji wote wa kigeni wamewapiga panga na waliosalimika na panga hilo ni golikipa Abel Dhaira na mshambuliaji mpya kutoka Burundi Amissi Tambwe.

Kiungo mkabaji Mussa Mudde aliyeitumikia klabu hiyo msimu uliopita na kumaliza msimu vibaya kwa kukosa penati kwenye mechi dhidi ya mahasimu wao Yanga Africa waliyolala kwa mabao 2-0 naye ameoneshhwa mlango wa kutokea kwenye klabu hiyo.

Sababu za kutemwa kwa wachezaji hao ni kutofikia kiwango ambacho kocha mpya wa klabu hiyo Abdallah Kibaden Mputa anakitaka kwa wachezaji wa kigeni.

Wengine ambao wamekumbana na panga hilo ni Mganda Assumani Buyinza,Samuel Ssenkoomi, MCongo Felix Cuipo na James Kun kutoka Sudan Kusini.

Mshambuliaji Felix Mumba Sunzu yeye amemaliza mkataba wake na klabu hiyo haina mpango wa kumuongeza mkataba mwingine

1 comment:

  1. Nimeipenda sana hii. kibadeni keep it up. unaposajili mchezaji wa nje lazima aonyeshe kiwango otherwise watakuwa wanawapa vilabu garama bila tija

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.