Mohamed Al Fayed amehitimisha miaka 16 ya kuimiliki klabu ya Fulham baada ya kuamua kuipiga bei kwa Shahid Khan.
Bilionea Khan, 62,anakuwa mmiliki wa sita MMarekani kumiliki timu za ligi kuu.
Al Fayed, 84,akiwa na asili ya Misri wakati wa umiliki wake aliiwezesha Fulham kutoka daraja la chini mpaka ligi kuu na kuiwezesha kucheza mpaka michuano mikubwa ya Ulaya.
Inaelezwa kuwa Fulham imeuzwa kwa dau la kati ya paundi milioni 150 mpaka paundi milioni milioni 200.
Msimu uliopita Fulham ilimaliza nafasi ya 12 kwenye ligi kuu ya Uingereza inayoshirikisha timu 20.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.