Thursday, July 25, 2013

SUAREZ mkono wa kwaheri

Mshambuluaji wa timu ya Liverpool ya England raia wa Uruguay Luis Suarez ana nafasi ndogo ya kuendelea kubaki kwenye timu hiyo baada ya kulazimisha kufanya mazungumzo na Arsenal,lakini historia yake pia inaonesha kuwa ana tabia ya kulazimisha kuondoka.

Suarez amewahi kuwa kwenye hali kama aliyokuwa nayo sasa wakati alipokuwa kwenye klabu yake ya kwanza barani Ulaya ya Groningen,ambao waliipiga chini ofa ya Ajax mwaka 2007, Suarez akaamu kuingia kisheria zaidi na timu yake ya wanasheria na kuipeleka klabu hiyo mahakamani.

Mshambuliaji huyo hakushinda kesi lakini ikailazimisha Groningen kukubali ofa nyingine ya Ajax waliporejea kwa mara nyingine japo haikufikia walipopataka lakini ilikuwa nzuri.
 
Dau lililowekwa lililomfanya Suarez kulazimisha kutaka kuzungumza na Arsenal inakwenda kwenye mtiririko kama wa Groningen kwakuwa tayari pia mshambuliaji huyo ameshawasiliana na mwanasheria wake ili kuona namna ambavyo anaweza kuondoka Liverpool.
Liverpool wameitolea nje ofa ya paundi milioni 40 iliyowekwa na Arsenal wakipandisha dau lake mpaka paundi milioni 55,thamani ambayo kocha Brendan Rogers anamfananisha na mshambuliaji mpya wa PSG Edinson Cavani aliyetokea Napoli.

Mkono wa kwaheri na ahsante kwa mashabiki
Haya mavitu mtayakosa

Kiduku nacho kinahusika

Suarez anataka kucheza Champions League mashindano ambayo Liverpool hawashiriki,lakini ni jambo la Arsenal kujiuliza kama wataweza kudumu na mshambuliaji huyo anayeonekana ni kawaida yake kushinikiza kuondoka kwenye timu pale anapoamua.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.