Monday, July 15, 2013
Kibaden kupitisha panga la "Ma Pro" Msimbazi
Kocha mkuu wa wa Wekundu wa Msimbazi Simba Abdallah Kibaden Mputa ndiye aliyeachiwa jukumu la kupiga panga wachezaji raia wa kigeni wanaotaka kusajiliwa na Wekundu hao katika kuimarisha kikosi hicho kwa msimu ujao wa ligi.
Kibadeni leo usiku anawasilisha majina ya wachezaji hao raia wa kigeni anaotaka kuwa nao kwa msimu ujao na wale ambao anaona wamekuja kutalii kwakuwa na uwezo mdogo ama uwezo wa kawaida tofauti na inavyotakiwa kwa mchezaji anayetoka nje ya nchi.
Wachezaji wanaofanya majaribio kwenye timu hiyo ambao bado hawana uhakika wa kusajiliwa ni Mganda Assumani Buyinza,Samuel Ssenkoomi, MCongo Felix Cuipo na James Kun kutoka Sudan Kusini.
Simba tayari wameinasa saini ya mshambuliaji namba moja wa timu ya Taifa ya Burundi Amissi Tambwe aliyejitia kitanzi cha miaka miwili kwa Wekundu hao.
Raia wa kigeni waliopo ndani ya kikosi cha wekundu hao ni golikipa Abel Dhaira na kiungo Mussa Mudde raia wa Uganda na inaendelea kusaka saini za wachezaji watakaoimarisha kikosi hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.