Thursday, July 11, 2013

Uganda yatua kuikabili Starz



Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes imetua nchini tayari kwa mechi ya kwanza ya kuisaka tiketi ya Fainali za mataifa bingwa barani Africa CHAN dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi Kuly 13 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

The Cranes imetua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ndege ya Air Uganda ambapo imefikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo.

Nao waamuzi wa mechi hiyo ambao wanatoka Burundi wamewasili kwa ndege ya Kenya Airways wakati Kamishna wa mechi hiyo Tesfaye Gebreyesus kutoka Eritrea yeye atatua kesho alfajiri kwa ndege ya EgyptAir.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.