Mashetani wekundu wa Manchester United wameikataa ofa ya Chelsea ya kutaka kumnasa mshambuliaji Wayne Rooney na wamesisitiza hauzwi.
Chelsea wamethibitisha kupeleka ofa ya United lakini wamekanusha kuwa walipeleka ofa ya fedha pamoja na kutaka kumtoa mmoja kati ya kiungo mchezeshaji Juan Mata au beki David Luiz.
Rooney amechukukizwa na
kuchanganywa na nafasi yake ndani ya kikosi hicho cha United baada ya bosi mpya
David Moyes kuweka wazi kuwa mshambuliaji huyo hatakuwa chaguo lake la
kwanza Old Trafford.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.