Sunday, July 14, 2013
Sharapova asaka maujuzi mapya
Mcheza tennis mwanamama anayeshikilia nafasi ya pili kwa ubora duniani Maria Sharapova amemtangaza bingwa mara nane wa Grand Slam Jimmy Connors kama kocha wake mpya.
Sharapova mwenye asili ya Russian,ambaye aliondolewa raundi ya pili kwenye michuano ya Wimbledon na Michelle Larcher de Brito amesema anaachana na huduma ya kocha wake Thomas Hogstedt na kumtakia kila la kheri akisema wamefanya kazi vizuri kwa muda wote aliokuwa akimfundisha.
Nani kwakwambia wacheza tennis sio warembo....
Kocha huyo mpya aliyetangazwa na Sharapova,Connors amewahi kumfundisha Andy Roddick akimsaidia kufika fainali ya US Open 2006,nusu fainali ya Australian Open 2007 na robo fainali ya Wimbledon na US Open 2007
Wakati akicheza Connors alishinda mataji matano ya US Open,akashinda taji la Wimbledon mara mbili na Australian Open mara moja na pia amewahi kukamata nafasi ya kwanza kwa ubora wa tennis kutokea July 1974 mpaka August 1977.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.