Sunday, July 21, 2013

Tegete aikomboa Yanga utumwani,Lutimba akiendelea kuvitesa vigogo

Mshambuliaji Jerryson Jerry Tegete ameikomboa Yanga kutoka kwenye utumwa wa URA baada ya kutupia bao la kusawazisha kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Taifa uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

URA ndio walikuwa wa kwanza kutupia wavuni mabao mawili yaliyopasiwa wavuni na mshambuliaji Lutimba Yayo kabla ya Didier Kavumbagu kutupia bao la kwanza kwa Yanga na Tegete akatupia bao la ukombozi lililofanya timu hizo kutoshana nguvu.

Mabao mawili ya Lutimba yamemfanya kuvitesa vigogo vya soka la Tanzania Simba na Yanga baada ya hapo jana pia kutikisa nyavu za Wekundu wa Msimbazi Simba.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.