Liverpool imeipiga chini ofa ya Arsenal iliyofikia paundi milioni 40 ili kumnasa mshambuliaji raia wa Uruguay Luis Suarez.
Dau hilo la paundi milioni 40 ilielezewa linafikia kipengele kinachomruhusu Suarez kuondoka kama timu yoyote itafikia kwenye dau hilo lakini hata hivyo Liverpool wamelitolea nje dau hilo.
Boss wa Liverpool Brendan Rodgers wiki iliyopita alisema thamani ya Suarez inalingana na ile ya mshambuliaji Edinson Cavani aliyenunuliwa na Paris St-Germain ya Ufaransa kwa dau la paundi milioni 55.
Real Madrid nao wanamtamani Suarez lakini mpaka sasa bado hawajawasilisha ofa yao.
Kuondoka kwa Suarez kulianza kutajwa mara baada ya kukumbana na adhabu ya kufungiwa mechi 10 baada ya kumtia meno beki wa Chelsea Branslav Ivanovic.
Aliwahi kukutana na adhabu mwaka 2011 baada ya kupatikana na hatia ya kumbagua Patrice Evra wa Manchester United.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.