Tuesday, July 16, 2013

EXCLUSIVE : Kizza bado kidooogo Yanga

Mshambuliaji Hamis Kizza Diego bado anaendelea na mazungumzo na klabu ya Yanga ili aweze kuanguka saini ya kuichezea klabu hiyo.

Awali kulikuwa kuna taarifa kuwa tayari mshambuliaji huyo amesaini mkataba mwingine wa miaka miwili kucheza kwa mabingwa hao wa Tanzania lakini ukweli ni kwamba bado hajaanguka saini.

Mabosi wa Yanga wanaendelea na mazungumzo na Kizza ili kuona kuwa anaongeza mkataba mwingine baada ya ule wa awali kumalizika.



Inaelezwa kuwa kuonekana na baadhi ya mabosi wa Yanga ni moja ya hatua zilizofikiwa baada ya kukubali kufanya mazungumzo ya kuendelea kubaki kwenye klabu hiyo na vibopa hao wanataka kumpa mkataba wa miaka miwili.

Kabla ya kutua Yanga Kizza ambaye ukitua Kampala anatambulika kama Diego amewahi kucheza kwenye timu ya Proline kabla ya kutimkia Uganda Revenue Authority URA mwanzoni mwa mwala 2009,akiisaidia klabu hiyo kushinda taji la ligi kuu ya Uganda akitupia wavuni mabao 17 na kuibuka kuwa mfungaji bora.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.