Rais wa Fifa Sepp Blatter anasema wako tayari kusogeza fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 zitakazofanyika Qatar.
Blatter amesema kwasasa bado muda unaruhusu kuweza kuisogeza michuano hiyo kutoka wakati wa joto mpaka msimu wa baridi ili kuondokana na malalamiko ya fainali hizo kuchezwa wakati wa joto kali.
Amesema wamepanga kufanya majadiliano mwezi October na kamati ya utendaji ya FIFA kuona uwezekano wa mabadiliko hayo ambayo yataathiri ligi nyingi.
Majira ya joto huko Qatar hali ya hewa hufikia mpaka nyuzi joto 50,japo wamepanga mechi hizo kupigwa kwenye viwanja vyenye viyoyozi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.