Sunday, July 14, 2013
Kamati ya utendaji TFF yabariki kamati mpya
Kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka nchini TFF inapitia majina ya kamati mpya zinazotarajiwa kutangazwa kesho ambazo zimepitishwa na mkutano mkuu wa dharula kama sehemu ya mabadiliko ya katiba ya TFF.
Kamati zilizopitishwa kwenye mkutano mkuu huo wa dharula ni pamoja na kamati ya rufaa ya uchaguzi na kamati ya maadili.
Kikao cha kamati ya utendaji kinaendelea hivi sasa kupitia na kubariki majina hayo ya kamati na baada ya hapo taratibu nyingine zitaendelea kuelekea kwenye uchaguzi wa TFF utakaofanyika mwezi September.
Mkutano mkuu wa dharula wa TFF tayari umepitisha mabadiliko ya katiba kama ilivyotakiwa na FIFA,mabadiliko ambayo awali yalileta utata kutokana na kufanyika kwa njia ya waraka ambayo ilipingwa na wadau wengi wa mpira wa miguu na baadaye serikali kuingilia kati kabla ya ujumbe wa FIFA kutua nchini na kuliweka sawa suala hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.