Tuesday, July 23, 2013

Rooney ajipeleka Chelsea


Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney amesafiri mpaka London na kujumuika kwenye klabu ya kucheza mchezo wa golf ya Queenwood iliyopo Surrey,ikiwa ni karibu kabisa na ulipo uwanja wa mazoezi wa Cobham ambako Chelsea wanafanya mazoezi na kuibua stori nyingine ya kwamba anasogea karibu na sehemu anayotaka kwenda kucheza.

Kwa Ulaya Queenwood Golf Club ni klabu ya upekee ambayo wanachama wake huingia kwa mualiko na kuna usiri wa kujua taratibu za kujiunga na ada inayotakiwa kulipiwa.

Habari hizo za Rooney kusogea karibu na Chelsea wanapofanya mazoezi itawashtua maboss wa United ambao wamesema mshambuliaji huyo anayelipwa paundi 240,000 kwa wiki hauzwi.

Hawa ndio Rooney anataka kucheza nao
Mourinho tayari amesema atamfanya Rooney chaguo la kwanza
Rooney ameshasema anataka kwenda zake darajani.

Itakumbukwa Rooney alipata maumivu wakati wa ziara ya United na akarudi Uingereza kwa matibabu na kuonekana kwake London kunaibua maswali mengine.

Mshauri wa mshambuliaji huyo hakukubali wala kukanusha kuhusiana na habari hiyo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.