Wednesday, July 24, 2013

Falcao agomea umri wake,asema wasimzeeshe


Mshambuliaji mpya wa Monaco ya Ufaransa Radamel Falcao amekataa uzee akisema umri anaozungumzwa kuwa nao ni wa uzushi.

Falcao raia wa Colombia aliyejiunga Monaco kwa dau la paundi milioni 53,imedaiwa ya kwamba amelipiwa dau kubwa wakati umri wake umekwenda ukifikia miaka 27.

Taarifa zaidi zinasema umri wa Falcao ni miaka miwili zaidi ya umri unaotajwa,kitu ambacho Falcao amejitokeza haraka na kukanusha.

Ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akisema ameshangazwa na stori kwenye vyombo vya habari kuhusiana na umri wake.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.