Monday, July 15, 2013

Man U watumbukia kwa Fabregas


Manchester United wametumbukia kwenye mbio za kumnasa kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas kwa dau la paundi milioni 25.

Dau hilo kwasasa linajadiliwa lakini inaelezwa kuwa linaoneka kuwa chini zaidi ya Barcelona wanavyomtathmini kiungo huyo wa zamani wa Arsenal ya England.

            Wacha nikacheze na Van Persie bwana...


Fabregas ametokea kwenye Academy ya Barcelona La Masia kabla ya kusajiliwa na Arsenal akiwa na miaka 16 mwaka 2003 na kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa klabu hiyo kabla ya kurudi tena Barcelona na sasa huenda akarejea tena kucheza soka huko England.

Akiwa Arsenal alicheza mechi 303 na kufunga mabao 57.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.