Golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania Juma Kaseja amepatiwa hati mpya ya kusafiria baada ya kupoteza ile ya awali aliyokuwa akiimiliki.
Akizungumza na blog ya Super Mario Kaseja amesema suala lake limeshughulikiwa vizuri na Uhamiaji baada ya kufuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwemo ya kutangaza kupotelewa na hati hiyo ya kusafiria.
Akifunguka zaidi Kaseja ameshukuru kupata hati nyingine ya kusafiria itakayomuwezesha kutumika kwenye mchezo wa kesho wa kuisaka tiketi ya fainali za mataifa bingwa barani Africa CHAN kama kocha Kim Paulsen atampanga kikosini.
Kaseja anasema hafahamu hati hiyo ameipotezea wapi licha ya kujitahidi kutazama katika maeneo yote aliyokuwepo ikiwemo nyumbani kwake ambako alilazimika kusakula kwenye kabati na maeneo mengine bila mafanikio.
Kaseja ndiye kipa chaguo la kwanza kwa kocha Kim Paulsen kwenye timu ya taifa na ndiye nahodha wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.