Friday, July 19, 2013

Man City wanafukuza mwizi kimya kimya,sasa ni zamu ya Jovetic


Manchester City ni kama wanafukuza mwizi kimya kimya ikiendelea kufanya usajili wake wa msimu ujao kiaina ikikusanya majembe na sasa ni zamu ya mkali wa Fiorentina Stevan Jovetic anayetua huko Etihad kwa dau la paundi milioni 22.

Jovetic raia wa Montenegro leo anafanyiwa vipimo vya afya na kukamilisha kuanguka saini yake ya kufunga ndoa rasmi na Man City chini ya kocha Manuel Pellegrini.

Jovetic, 23,pia alikuwa anawaniwa na Arsenal,Manchester United na Chelsea zote za England.


• Stevan Jovetic

  • Born: Titograd, 2 November, 1989
  • Nickname: The Montenegrin Messi
  • Clubs: Mladost Podgorica, Partizan Belgrade, Fiorentina
  • International: Montenegro - 27 caps, 10 goals
City tayari pia imemalizana na Alvaro Negredo kutoka Sevilla ya Hispania hapo jana.

Alvaro Negredo

  • Born: Madrid, 20 August, 1985
  • Nickname: La fiera de Vallecas (The beast of Vallecas)
  • Clubs: Rayo Vallecano, Real Madrid, Almeria, Sevilla
  • International: Spain - 14 caps, six goals

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.