Jembe Didier kazini akiwa na Galatasary
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba ametangaza kuwa atajenga hospitali tano kwenye ardhi ya nyumbani kwao nchini Ivory Coast ambazo zinalenga afya za watoto na wanawake.
Katibu Mkuu wa Didier Drogba Foundation, Guy Roland Tanoh,amesema mradi huo utagharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 5 ambazo zitatumika kujenga hospitali hizo kwenye miji ya Abidjan, Yamoussoukro, Man, Korhogo na San Pedro.
Mpaka sasa wamefanya Harambee ya kuchangisha kiasi cha dola za kimarekani milioni 4 na dola milioni moja iliyobakia haitakuwa tatizo kwao.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.