Wednesday, July 17, 2013
CAF yawachelewesha Al Ahly na Zamalek
Shirikisho la soka barani Africa CAF limechelewesha pambano la mahasimu wa soka la Misri Zamalek na Al Ahly ukiwa ni mchezo wa kufungua raundi ya hatua ya makundi ligi ya mabingwa Africa mpaka Jumatatu ijayo.
Wakubwa hao wa Misri ilikuwa wapambane Jumapili huko El Gouna city kilomita 500 kutoka jijini Cairo kwasababu za kiusalama.
Zamalek imethibitisha kupewa taarifa na CAF kuhusu kuutumia uwanja wa El Gouna japo haukuwa mmoja wa viwanja ilivyovichagua kucheza mechi zake za michuano hiyo na pia wamethibitisha mchezo kusogezwa mbele kwa saa 24.
Waziri wa mambo ya ndani wa Misri aligoma kuruhusu mchezo huo kuchezwa Cairo au Alexandria kabla ya Zamalek kulazimika kufanya chaguo la tatu la kucheza El Gouna.
Kocha mkuu wa Zamalek Helmy Tolan amesema sasa timu hiyo itasafiri kwenda El Gouna Ijumaa badala ya kesho Alhamis.
Hata hivyo haikuwekwa bayana kama mchezo huo utaruhusu mashabiki kuingia uwanjani kushuhudia.
Wakati huohuo kikundi cha mashabiki cha Al Ahly "Ultra Ahlawy" na kikundi cha mashabiki cha Zamalek "Ultra White Knights" wametangaza kuwa tayari kuwasaidia Polisi kuhakikisha usalama wa mchezo huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.