Wednesday, July 24, 2013

EXCLUSIVE : Mgosi atesa China,arejea kufanya yake ligi kuu,asema Simba na Yanga hapana

Mshambuliaji wa zamani wa Simba Mussa Hassan Mgosi amerejea kutoka nchini China alikokwenda kushiriki mashindano maalumu ya mataifa ya Africa,na kutamka kuwa hataki kucheza timu kubwa kwa sasa katika ligi kuu ya Tanzania bara inayotarajia kuanza kuunguruma August 24.

Mgosi ambaye ameibuka kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo ya mataifa ya Africa yaliyochezwa kwa mwezi mmoja akitupia wavuni mabao 14 amesema yupo kwenye mazungumzo na timu kadhaa zinazohitaji huduma yake kwa msimu ujao wa ligi na miongoni mwao hakuna Simba wala Yanga ambazo kwasasa hataki kuzisikia.

Amesema msimu ujao ataendelea kung'ara katika ligi kuu lakini itakuwa si katika timu yoyote kubwa kwakuwa sasa hataki kucheza mpira kwa presha.

Katika mashindano hayo Tanzania imeibuka na ubingwa kwa mara ya pili mfululizo,baada ya kushinda mechi zake zote ilizoshuka dimbani.

Walifungua pazia kwa kucheza na Senegal wakashinda mabao 3-1,wakaifunga Nigeria 2-1 kabla ya kuipa kipigo Mali cha mabao 4-2 na kutinga nusu fainali ambako waliifumua Kenya 3-1 na katika fainali wakaishindilia Guinea mabao 3-1 huku Mgosi akitangazwa mchezaji bora na mfungaji bora wa mashindano.
 




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.