Wednesday, July 17, 2013

Rooney na Moyes hakieleweki



Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney amechukukizwa na kuchanganywa na nafasi yake ndani ya kikosi hicho baada ya bosi mpya David Moyes kuweka bayana kuwa mshambuliaji huyo hatakuwa chaguo lake la kwanza Old Trafford.

Rooney, 27,ameelezea hisia zake za kukatishwa tamaa na amesema wazi kuwa hatakubaliana na mtindo wa kucheza kwa mzunguko tena akiwa chaguo la pili nyuma ya Mholanzi Robin van Persie.

Mshambuliaji huyo wa England amebakisha miaka miwili katika mkataba wake wa sasa na tayari amehusishwa kutakiwa na klabu za Chelsea na Arsenal.

Rooney katika moja ya shughuli zake...

Mtanikumbuka me sio wa kukaa bench

Rooney na Moyes wamewahi kuingia kwenye mgogoro wakati mshambuliaji huyo alipokuwa Everton na alipouzwa bila ridhaa yake,mgogoro wao ulifika mpaka mahakamani na Rooney akatakiwa kumuomba radhi Moyes ikiwa pamoja na kumlipa faini.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.