Wednesday, July 24, 2013

MOURINHO : Presha iko Man City

Bosi wa Chelsea Jose Mourinho anasema katika msimu ujao wa ligi kuu ya England presha itakuwa kwa Manchester City baada ya kumwaga fedha kwenye usajili.

Bosi mpya wa Man City Manuel Pellegrini amewashusha kikosini nyota wa Hispania Alvaro Negredo na Jesus Navas kutokea Sevilla,Stevan Jovetic kutokea Fiorentina na Fernandinho kutokea Shakhtar Donetsk akitumia paundi milioni 80.

Mourinho anaamini kwa uwekezaji walioufanya kuchukua wachezaji wazoefu ina maana watu wanatarajia makubwa kutoka kwa Man City kuliko kwa Chelsea iliyosajili vijana.


Chelsea wamewasaini makinda Marco van Ginkel na Andre Schurrle,na Mourinho anasema kuchukua taji la EPL itakuwa sherehe kubwa kwake na itakuwa ya kipekee.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.