Tuesday, July 16, 2013

Ivanovic amsafishia njia Suarez Chelsea


Beki wa Chelsea MSerbia Branislav Ivanovic amesema hana bifu na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez na akimtaja mchezaji huyo kama mmoja wa washambuliaji bora katika ligi kuu ya Uingereza EPL.

Maneno hayo ya Ivanovic yanaweza yakawa yanafungua na kusafisha njia kwa Suarez kutua darajani baada ya kuwepo taarifa kuwa anataka kuondoka na Chelsea ni moja ya vilabu vinavyotamani huduma yake.


Suarez, anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi 10 baada ya kumng'ata Ivanovic kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza mwezi April.

Inaelezwa kuwa Chelsea ni moja ya sehemu sahihi kwa mshambuliaji huyo kutua kama akiondoka Liverpool na Ivanovic anasema atajisikia furaha kucheza pamoja na Suarez na anasema kila kilichotokea uwanjani kilibaki uwanjani.

Vilabu vingine vinavyotajwa kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo ni pamoja na Arsenal,Real Madrid,PSG na Bayer Munich.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.