Wekundu wa Msimbazi Simba wameendeleza uteja mbele ya timu ya mamlaka ya mapato ya Uganda URA baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao lililowekwa wavuni na Betrum Mombe katika dakika ya 8,bao lililodumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili URA wakaingia na kasi mpya na kufanikiwa kuendeleza ubabe wao mbele ya Simba kwa mabao yaliyotupiwa wavuni na Ngama Emmanuel katika ya 60 na Lutimba Yayo dakika ya 76
Simba tokea imeanza kucheza na URAkatika michezo mbalimbali ya kirafiki na mashindano imekuwa inakutana na kipigo na ushindi wake ni sare mbele ya wababe hao wanaokusanya kodi Uganda,na kipigo cha leo kimeendeleza uteja wao.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.