Tuesday, July 16, 2013

Aliyeipa ubingwa wa AFCON Super Eagles kutimkia Ulaya


Timu ya Warri Wolves ya Nigeria imefikia makubaliano na mahasimu wao Enugu Rangers kuhusiana na uhamisho wa kiungo mshambuliaji Sunday Mba.

Kiungo mshambuliaji huyo mwenye miaka 24 ambaye alitupia wavuni bao la ushindi lililowapa ubingwa wa AFCON Nigeria Super Eagles mapema mwaka huu ataendelea kumilikiwa na Warri lakini atacheza kwa mkopo Enugu mpaka mwisho wa msimu mwezi September.

Haina uhakika kama Mba atarejea Warri baada ya kumalizika msimu huu kwakuwa anatarajia kusaka timu barani Ulaya na huenda mpango huo ukakamilika wiki zijazo.

Makubaliano hayo yamemaliza utata wa nani anammiliki mchezaji huyo kati ya vilabu hivyo viwili.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.