Monday, July 22, 2013

Mabao ya Sunzu yawindwa Zanaco

Mshambuliaji aliyemaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi Simba ya Tanzania Felix Mumba Sunzu anawindwa na timu ya Zanaco ya Zambia.


Sunzu,kaka wa shujaa wa Zambia aliyewapa ubingwa wa Africa 2012 Stopilla Sunzu,alikuwa akiitumikia Simba kwenye msimu uliopita ambao kwake hakuumaliza vizuri baada ya kukutana na magumu ya kusimamishwa kuitumikia timu hiyo baada ya kutofautiana na kocha raia wa Ufaransa Patrick Liewig ambaye naye ameoneshwa mlango wa kutokea kwenye timu hiyo.

Katibu mkuu wa Zanaco Jordan Maliti amethibitisha kuwa wanahitaji huduma ya mshambuliaji huyo kwaajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Zambia ikitambulika kama Faz Super League.

Anasema wamejaribu kuwasiliana naye lakini bado imekuwa ngumu kumalizana naye kabla ya kwenda kuweka kambi huko Livingstone.


Sunzu amewahi kucheza kwenye timu ya Marsa ya Tunisia na Al Hilal ya Sudan,alitua Simba ya Tanzania akitokea Al Hilal na ndiye alikuwa mchezaji ghali zaidi katika timu hiyo ya Simba akilipwa mshahara mkubwa zaidi ya wachezaji wote,akilipwa dola 3500.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.