Friday, July 19, 2013

Mourinho amlazimisha Moyes kuzungumza


Kocha wa Manchester United David Moyes kwa mara nyingine amelazimika kuzungumza akiwa huko Sydney kuhusiana na sakata la mshambuliaji Wayne Rooney na kusisitiza kuwa hauzwi ikiwa ni siku moja baada ya Chelsea kusema mshambuliaji huyo ndiye pekee wanayewania saini yake.

Bosi huyo wa United amesema maamuzi ya klabu hayabadiliki na tayari wameweka wazi kuwa hawatampiga bei na wanarudia tena kusisitizwa kuwa hatapigwa bei.

Tayari bosi wa Chelsea Jose Mourinho amekwishaweka bayana kuwa wamepeleka ofa ya kutaka kumsajili Rooney huku akimchochea kuondoka kwa kusema hawezi kupata namba kwenye timu ya taifa ya England kama ataendelea kubaki United kama mshambuliaji chaguo la pili.

Wakati huo huo Moyes bado ana imani ya kumnasa kiungo Cesc Fabregas licha ya vijembe vya kocha wa Arsenal Arsene Wenger ambaye anasema United wanajisumbua.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.