Friday, July 12, 2013
Mourinho aendelea kumtamani Rooney
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amekiri kuwa bado anamtamani mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney ambaye yeye ni mshabiki wake mkubwa.
Hata hivyo Mourinho anasema kwasasa hawezi kuzungumza kwa undani kuhusiana na mshambuliaji huyo kwakuwa bado ni mchezaji halali wa Manchester U.
Iko siku siku utakuwa mshambuliaji wangu
Hatima ya Rooney bado haieleweki kufuatia kuwepo kwa minong'ono ya kutaka kuondoka kwa mashetani wekundu hao wa Manchster United ingawa boss mpya David Moyes anasema mshambuliaji huyo hauzwi.
Mara kadhaa Rooney ameingia kwenye mgogoro na kocha aliyestaafu Alex Ferguson na pia ameshawahi kuomba kuondoka wakati wa utawala wa babu huyo.
Hapa alikuwa akimuhakikishia namba Cech ya kusimama langoni
Mourinho pia amekiri kuwa kusajiliwa kwa kipa mkongwe Mark Schwarzer kutaleta changamoto kwa golikipa Petr Cech ambaye anasema ataendelea kubakia kuwa chaguo lake la kwanza.
Amemtaka kipa huyo mkongwe aliyetua akitokea Fulham kukaza msuli na kuleta ushindani kwa Cech kwakuwa hana shaka kuwa Cech ndiye kipa wake chaguo la kwanza kukaa langoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.