Monday, July 15, 2013

Cavani huyoooooo PSG,anaandikisha rekodi mpya


Edinson Cavani yupo zake Paris kukamilisha taratibu za kuhamia Paris Saint-Germain,kwa dau linalodaiwa kufikia Euro milioni 64 ambalo litavunja rekodi ya usajili Ufaransa.

Cavani mwenye miaka 26 aliyeibuka kuwa mfungaji bora msimu uliopita wa ligi kuu ya Italia Serie A akitupia wavuni mabao 29 akiwa na Napoli ametua leo huko Paris tayari kukamilisha usajili wake.
                                              Cavaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii....

Mapema asubuhi leo Mkurugenzi wa ufundi aliyetangaza kuachana na klabu ya PSG Leonardo alionekana kwenye hotel na mshauri wa mshambuliaji huyo anayefahamika kwa jina la utani la "The Matador".

Cavani anatakiwa kwanza kufaulu vipimo vya afya kabla ya kujitia kitanzi cha miaka mitano ambako atacheza timu moja na mchezaji mwenzake waliyewahi kucheza naye Napoli MuArgentina Ezequiel Lavezzi.

                 Mtanitambuaje makipa wa League 1


Rekodi ya sasa ya uhamisho kwenye ligi kuu ya Ufaransa Le Championate inashikiliwa na MColombia Radamel Falcao aliyesajiliwa na Monaco hivi karibuni kwa dau la Euro milioni 60 akitokea Atletico Madrid ya Hispania.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.