Saturday, July 13, 2013
Starz majanga
Bao lililofungwa na Dennis Iguma limetosha kuipa ushindi wa bao 0-1 timu ya Taifa ya Uganda The Cranes mbele ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Starz kwenye mchezo wa kuisaka tiketi ya fainali za mataifa bingwa barani Africa CHAN.
Ushindi huo unawaweka pazuri Uganda Cranes ambao watakuwa nyumbani Kampala kwenye dimba la Nelson Mandela kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa July 27,mchezo utakaoamua timu itakayotinga kwenye fainali za CHAN zitakazochezwa nchini Africa Kusini.
Washambuliaji wa Taifa Starz wanapaswa kujilaumu kwa kukosa umakini na mashambulizi yao yakawa yanaishia kwa mabeki wa Cranes iliyokuwa chini ya nahodha Hassan Waswa ama mikononi mwa golikipa Hamza Muwonge.
Safu ya ushambuliaji ya Starz iliyokuwa chini ya Mrisho Ngassa na John Bocco ilionekana kupwaya na kufanya pengo la Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kuonekana wazi.
Samatta na Ulimwengu wanaocheza Tp Mazembe ya Congo DRC hawaruhusiwi kucheza michuano hiyo kwakuwa inahusisha wachezaji wanaocheza kwenye ligi ya ndani peke yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.