Monday, July 22, 2013

Pazia ligi kuu kufunguliwa August 24,Simba,Yanga uso kwa uso October 20


Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Tanzania Bara msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa timu zote 14 kushuka dimbani katika miji saba tofauti.

Wakongwe wa soka la Tanzania na mahasimu wa jadi Simba na Yanga wanatarajia kukutana uso kwa uso October 20 kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na shirikisho la soka nchini TFF.

Mchezo huo ndio utakuwa wa kwanza kwa msimu huu kwa vigogo hao kukutana.


Kabla ya ligi hiyo kuanza kutakuwa na mechi ya kufungua msimu (Ngao ya Jamii- Community Shield) kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu bingwa Azam itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi za Agosti 14 mwaka huu zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).

Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).

Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa pili utamailizika Aprili 27 mwakani.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.