Mkimbiza upepo wa Marekani Tyson Gay na MJamaica aliyewahi kushika rekodi ya dunia ya mbio za mita 100 Asafa Powell wamethibitika kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni.
Gay, 30,alielezwa na US Anti-Doping Agency kuwa vipimo vilivyochukuliwa mwezi May vinaonesha kutumia dawa hizo wakati uongozi wa Powell nao umethibitisha kuwa mwanariadha huyo amethibitika kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni.
Mbio zetu zote hizi bila dawa za kuongeza nguvu hatuwezi....
MJamaica mwingine Sherone Simpson,naye pia amethibitika kutumia dawa hizo zisizoruhusiwa michezoni.
Kupimwa kwa Powell na Simpson kumekuja mwezi mmoja baada ya MJamaica bingwa wa Olympic Veronica Campbell-Brown kuthibitika kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni.
Powell ndiye alikuwa wa mwisho kushikilia rekodi binafsi ya mbio za mita 100 kabla ya utawala huo kuchukuliwa na MJamaica mwenzake Usain Bolt aliyeivunja rekodi hiyo mwaka 2008.
Powell baadaye aliisaidia Jamaica kushinda dhahabu kwenye mbio za mita 400 kwenye Oympic mwaka 2008 huko Beijing.
Mimi ndio mwenyewe bwana,achana na hao,wananiita Bolt
Vinara wa kasi duniani kwa mbio za mita 100
- Usain Bolt (Jam) - 9.58 secs
- Tyson Gay (USA) - 9.69 secs
- Yohan Blake (Jam) - 9.69 secs
- Asafa Powell (Jam) - 9.72 secs
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.