Wednesday, November 20, 2013

Zlatan asusia kutazama kombe la dunia

Nahodha wa Sweden Zlatan Ibrahimovic amesema hatatazama fainali za kombe la dunia baada ya kupoteza mbele ya URENO hapo jana.

Mshambuliaji huyo wa Paris St-Germain alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa jana lakini Cristiano Ronaldo akapiga hat-trick na kuifanya Ureno kutinga kwenye fainali za kombe la dunia kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-2.

Ibrahimovic, 32,amesema kitu cha uhakika fainali za kombe la dunia bila uwepo wake hawezi kuzifuatilia huku akiipongeza Ureno akisema timu zote zilistahili kwenda kwenye fainali za kombe la dunia.
Mchezo huo wa hatua ya mtoano kati ya Sweden na Ureno ambazo zote zilimaliza nafasi ya pili kwenye hatua ya makundi ilichukuliwa ni kama mpambano wa Ibrahimovic na Ronaldo wawili kati ya wachezaji bora duniani.

Na wawili hao ndio walifunga mabao yote sita katika mechi mbili walizokutana.

Zlatan mshambuliaji wa zamani wa Inter Milan ambaye amecheza kwenye fainali mbili za kombe la dunia amefunga mabao nane kwenye michezo ya kufuzu ukijumuisha na hatua ya mtoano na amesaidia kufungwa kwa mabao mengine sita kati ya mabao yao 21.
Kwa upande wake Ronaldo anayechezea Real Madrid,ambaye amefunga mabao 34 katika michezo 24 msimu huu kwa klabu yake na timu ya taifa amesema amefanya kazi yake ambayo ndio lengo lake la siku zote.

Kwasasa ni mmoja wa wafungaji wanaoongoza kwa kuzifumania nyavu Ureno akiungana na mshambuliaji wa zamani wa PSG Pauleta wakiwa na mabao 47.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.