Lionel Messi ametupia wavuni mara mbili wakati Barcelona ikikata tiketi ya kutinga hatua ya mtoano ya Champions League
wakipata ushindi wa mabao 3-1 mbele ya AC Milan.
Messi amefunga bao lake la kwanza baada ya michezo minne huku bao la kwanza akifunga kwa penati baada ya Neymar kufanyiwa madhambi na Ignazio Abate.
Sergio Busquets akafunga bao la pili akimalizia kazi ya Xavi kabla ya Kaka kupiga mpira ambao Gerard Pique akajifunga na kufanya kuwa 2-1 na Messi akatupia bao la tatu ambalo liliipa Barca ushindi wa mabao 3-1 na kuikata tiketi ya hatua ya mtoano.
Matokeo ya mechi zote za jana Champions League
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.