Friday, November 1, 2013

VPL : Yanga yakaa kileleni,yaifanya mbaya JKT Ruvu


Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara Yanga Africa wamekwea kileleni mwa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kuwachapa maafande wa JKT Ruvu kwa mabao 4-0 kwenye uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo yamefungwa na Mrisho Ngassa aliyefunga mawili na mengine yakiwekwa wavuni na Oscar Joshua na Jerry Tegete.

Ushindi huo umewafanya Yanga kufikisha pointi 25 ikiwa ni pointi mbili mbele ya Azam Fc na Mbeya City wenye pointi 23 lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi ambayo Azam wanacheza kesho na Ruvu Shooting wakati Mbeya City wanawakaribisha Ashanti United kwenye uwanja wa Sokoine.

Huu ni ushindi mwingine mkubwa kwa Yanga baada ya kushinda mabao 3-0 kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Mgambo Shooting.

Ngassa sasa amefikisha mabao 5 katika orodha ya wafungaji wa ligi kuu.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.