Thursday, November 14, 2013

Iniesta aingia kwenye rada za Moyes


David Moyes anafikiria mwaka mpya kutumbukia kumfukuzia kiungo wa Barcelona Andres Iniesta baada ya kudokezwa bifu la chinin chini kati ya kiungo huyo na maboss wa Nou Camp.

Bosi huyo wa Manchester United anafuatilia kwa umakini na anaweza kutumbukiza ofa wakati wa usajili wa dirisha dogo mwezi January.


Tayari inazungumzwa kuwa kiungo huyo aliyedhaaniwa kuwa anaweza kuwa kwa muda mrefu ndani ya Barcelona anafikiria kusaka timu nyingine kuliko kuongeza mkataba kufuatia vugu vugu hilo linaloendelea dhidi ya mabosi.

Moyes anaona kiungo huyo anaweza kumsaidia zaidi baada ya kiungo Manuel Fellaini aliyemchukua Everton kushindwa kufanya makubwa mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.