Schalke walianza vizuri mchezo huo wakikosa kosa kupitia kwa Julian Draxler na Adam Szalai lakini Chelsea wakatangulia kufunga baada ya mpira uliopigwa na golikipa Timo Hildebrand kugongwa na Eto'o na kutumbukia wavuni.
Eto'o akatupia bao la pili akimalizia kazi nzuri ya kiungo MBrazil Willian ambaye nyota yake ilingára katika mchezo huo kabla ya Demba Ba kumalizia kazi akitupia bao la tatu.
Ushindi huo kwa Chelsea unawafanya kujitawala kileleni kwa tofauti ya pointi tatu na kuendelea kuongoza kundi E na sasa wanahitaji sare katika mchezo unaofuata dhidi ya FC Basel ili kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya mtoano.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.