Wednesday, November 6, 2013
Lewandowski athibitisha kuondoka Dortmund
Mshambuliaji raia wa Poland Robert Lewandowski amethibitisha kuwa ataondoka Borussia Dortmund ifikapo mwishoni mwa msimu ili kupata uzoefu mpya bila ya kuweka bayana anapotimkia.
Dortmund wanakutana na Arsenal leo katika Champions League,lakini Lewandowski mwenye miaka 25 amesema ataondoka wakati mkataba wake utakapomalizika mwezi June.
Mshambuliaji huyo alijiunga Dortmund July 2010 na anasema anajisikia vizuri akiwa kwenye klabu hiyo lakini ameamua kusaka uzoefu mpya msimu ujao lakini juu ya wapi anakwenda atatangaza maamuzi yake mwakani.
Msimu uliopita akiwa mchezaji wa kwanza kufunga goli nne kwenye Champions league hatua ya nusu fainali ,Lewandowski tayari ametupia wavuni mabao 9 kwenye michezo 11 ya ligi msimu huu.
Kwa mujibu wa sheria za FIFA , Lewandowski anaweza kutangaza maamuzi yake anakokwenda kuanzia January 1 na anahusishwa kutimkia Bayern Munich,ambako alitaka kwenda mwishoni mwa msimu uliopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.