Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi atakaa nje ya dimba kwa wiki sita mpaka nane kwasababu ya majeruhi.
Messi alipata mushkeli ya misuli kwenye mchezo wao dhidi ya Real Betis.
Mshambuliaji huyo raia wa Argentina amekuwa na msimu mbaya itakumbukwa mwezi August alitolewa kwenye mchezo dhidi ya Atletico Madrid na akaumia mwezi September kwenye mchezo dhidi ya Almeria.
Taarifa ya Barcelona imethibitisha Messi kukaa nje kwa wiki sita mpaka nane.
Hilo lina maana kuwa Messi ataukosa mchezo wa kirafiki Argentina dhidi ya Ecuador na Bosnia & Herzegovina mwezi huu pamoja na mechi kadhaa za ligi kuu ya La liga na atakosa michezo miwili ya hatua ya makundi champions league dhidi ya Ajax na Celtic.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.