Mshambuliaji Elius Maguri ameendeleza kasi ya kuzichungulia nyavu baada ya kutupia wavuni bao pekee wakati Young Future Taifa Starz wakiikamua Taifa Starz.
Maguri anayeichezea Ruvu Shooting ameendeleza kasi yake ya kutupia wavunikama ilivyo kwenye ligi kuu ambako ana magoli 9 nyuma ya Amis Tambwe wa Simba anayeongoza akiwa na magoli 10.
Mchezo huo wa leo umetumiwa na kocha mkuu wa Stars Kim Paulsen kuteua kikosi cha Taifa stars atakachokitumia wakati wa mchezo wa kimataifa wa kujipima nguvu kabla ya kuwachuja kwa mara nyingine kuwapata wachezaji watakaounda Kilimanjaro stars itakayokwenda nchini Kenya kushiriki michuano ya kombe la Chalenji itakayoanza Novemba 27 mpaka December 12 mwaka huu.
Stars kesho inataraji kukwea pipa kuelekea Arusha kujiandaa na mchezo huo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.