Thursday, November 21, 2013

Fifa yalipeleka soka Digitali


Fifa imesema imepanga kutumia spray maalumu kuweka mstari wa ukuta unaowekwa kabla ya kupigwa adhabu kwenye klabu bingwa ya dunia ya vilabu itakayofanya maisha yawe rahisi kwa waamuzi na kuondoa kadi za njano.

Katika taarifa yake FIFA imesema spray hiyo itatumika kwenye klabu bingwa ya dunia ya vilabu itakayoanza December 11-21 nchini Morocco baada ya majaribio kwenye fainali za dunia chini ya miaka 20 na miaka 17.

Spray hiyo ambayo hupotea baada ya dakika moja itakuwa inapulizwa uwanjani kuchora mstari wa kupanga ukuta wa timu inayopigiwa adhabu,kitu ambacho kitaondoa kadi za njano ambazo hupewa mchezaji anayekaidi maamuzi ya mwamuzi ya kuonesha sehemu ya kuweka ukuta wa kulinda lango lao.

Klabu bingwa ya dunia ya vilabu itazihusisha Bayern Munich ya Ujerumani, Atletico Mineiro ya Brazil,Guangzhou Evergrande ya Misri,Al-Ahly ya Misri,Monterrey ya Mexico,Auckland City ya New Zealand,na Raja Casablanca ya Morocco.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.