Wednesday, November 6, 2013

Modric : Chelsea,United ,PSG wote wananizimia

Nyota wa Real Madrid Luka Modric amedai kuwa timu za Chelsea, Manchester United na PSG zote zilijaribu kumsajili.

Nyota huyo wa Real Madrid amesema timu hizo zilionesha nia ya kumsajili baada ya kuwa wakati mgumu katika mwaka wake wa kwanza aliotua Madrid.


Modric anasema kabla ya kuondoka Tottenham,kocha wa sasa wa Madrid Carlo Ancelotti alijaribu kumnasa aili acheze Chelsea na baadaye PSG.
Lakini Modric pia anasema hata Sir Alex Fergusson alitaka kumnasa atue United huku pia akimtaja kocha mpya wa United David Moyes pia kutamani huduma yake kwenye usajili uliopita.

Moyes akalazimika kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Everton na kumnasa Marouane Fellaini kwa dau la paundi milioni 27.5.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.