Monday, November 11, 2013
Sikia maneno ya Moyes kuhusu ubingwa
Kocha wa Manchester United David Moyes ametabiri kuwepo kwa changamoto ya karibu ya kuwania taji la ligi kuu ya Uingereza baada ya ushindi wao wa jana dhidi ya Arsenal.
Ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Robin Van Persie limeifanya Manchester United kuwa na tofauti ya pointi tano na wanaoongoza ligi hiyo Arsenal wakati Chelsea, Manchester City na Tottenham wote wakidondosha pointi kwenye michezo yao.
Moyes anasema ligi ya msimu huu itakuwa na mshtuko na hakuna anayeweza kulikimbia hilo.
United walianza kwa kusuasua msimu huu na kuzua maswali juu ya uwezo wa Moyes aliyemrithi Sir Alex Ferguson mwezi July.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.