Yanga usiku wa kuamkia leo imemsainisha mkataba wa miaka mitatu kiungo wa Ruvu Shooting Hassan Dilunga.
Afisa habari wa Ruvu Shooting Massau Bwire anasema Dilunga bado ana mkataba wa miaka miwili na klabu yao na hawaelewi ni kwa namna gani Yanga wamemsajili.
Yanga Africa kupitia Afisa habari wake Baraka Kizuguto wamethibitisha taarifa ya kumsainisha Dilunga kwa miaka mitatu na wakisema wanajua walichokifanya.
Kizuguto amesema wanafanya mambo yao kwa uhakika na hawana wasiwasi wowote na Dilunga sasa ni mchezaji wao halali.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.