Thursday, November 14, 2013

Zabaleta aibua balaa Man City kisa kunyangánywa unahodha


MANUEL PELLEGRINI amemtosa unahodha msaidizi Pablo Zabaleta hali iliyoibua mgogoro kwenye vyumba vya kubadilishia.

Nyota huyo wa Argentina amekuwa akivaa kitamba cha unahodha kuchukua nafasi ya majeruhi Vincent Kompany tokea enzi za Roberto Mancini lakini Pellegrini amamtosa Zabaleta na nafasi amepewa Yaya Toure.
Toure amekuwa akikiongoza kikosi hicho kwa wiki za hivi karibuni kutokana na Kompany kuwa nje lakini maamuzi ya Pellegrini kumnyangánya kitambaa cha unahodha Zabaleta kimewaumiza wachezaji kadhaa.

Baadhi ya wachezaji wameshangazwa kwa Zabaleta kunyangánywa cheo hicho cha unahodha msaidizi huku ikielezwa ni mchezaji mwenye nguvu na mwenye kuungwa mkono hata na wachezaji vijana.
Wachezaji walioshtushwa na taarifa hiyo wamesema ,Yaya ni mchezaji wa kiwango cha dunia,mmoja wa wachezaji bora lakini hana sauti kwa wachezaji kama ilivyo Zabaleta.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.