Arsene Wenger amechoshwa na Olivier Giroud katika sehemu ya mashambulizi na sasa anataka kumgeukia mshambuliaji wan Chelsea Demba Ba.
Ba anaweza kunaswa na Arsenal kwa paundi milioni 15 baada ya kushindwa kumsajili kwenye usajili uliopita wa majira ya joto.
Wenger alijaribu kumnasa Ba, 28,Gonzalo Higuain, Luis Suarez na Karim Benzema lakini wote akawakosa.
Ba alifunga goli lake la kwanza kwa Chelsea msimu huu kwenye mchezo wa champions league dhidi ya Schalke lakini bado hana nafasi kubwa huko Stamford Bridge.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.