Ivory Coast watacheza dhidi ya Senegal ,wakati Nigeria watakuwa wenyeji wa Ethiopia huku Algeria wakicheza dhidi ya Burkina Faso.
Anasema ukiwatazama kama Ivory Coast wapo kwenye kiwango cha juu na wanaweza kuifunga timu yoyote kwahiyo ukiwatazama unaona hawana ugumu kufuzu kwenye fainali hizo za dunia.
Akiwazungumzia Nigeria,Shehata anasema itakuwa ngumu kwa Ethiopia kufuzu kupitia mgongo wa Super Eagles akitazama hata kwa upande wa uzoefu kwa wachezaji baina ya vikosi hivyo viwili na tena mchezo ukichezwa nyumbani kwa Nigeria huko Calabar.
Licha ya Algeria kufungwa 3-2 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Burkina Faso lakini anawapa nafasi ya kusonga mbeloe kwasababu ya uzuri wa kikosi chao ambacho kiliweza kufunga mabao mawili kwenye mchezo huo wa kwanza.
Pia akaigusia Misri The Pharaos akisema ni ngumu kwao kufuzu baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa Ghana.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.