Baada ya kumsimaisha mwenyekiti Ismail Aden Rage,kamati ya utendaji ya Simba imelivunja benchi la ufundi lililokuwa chini ya kocha Abdallah king Kibaden na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo Julio.
Kamati hiyo ya utendaji imefikia maamuzi hayo katika kikao cha jana ambacho pia kilikubaliana kumsimamisha mwenyekiti wao Rage mpaka mkutano mkuu wa wanachama utakapofanyika ambako anatakiwa kujieleza mbele ya wanachama.
Nafasi ya Kibaden na Julio sasa inachukuliwa na kocha wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya Zdravko Logaruzic raia wa Croatia ambaye atasaidiwa na Suleiman Matola aliyekuwa kocha wa Simba B.
Tokea mzunguko wa kwanza umemalizika mabosi wa Simba hawakuridhika na mwenendo wa timu yao na kikao cha jana kikafikia maamuzi hayo magumu.
Nafasi ya mwenyekiti sasa atakaimu Joseph Itangáre Kinesi na makamu wake atakuwa Swedy Nkwabi ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji.
Simba wanakamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.