Friday, November 8, 2013

Azam FC yakatisha mkataba wa Stewart,yaanza mchakato wa kutangaza mrithi wake


Azam FC na kocha raia wa Uingereza Stewart John Hall wamekubaliana kiungwana kusitisha mkataba baada ya mchezo wa jana.

Taarifa ya Azam kupitia kwenye mtandao wa klabu hiyo imesema kuwa pande zote mbili zimefikia makubaliano kwaajili ya maendeleo ya Azam FC yenye lengo la kukua zaidi na kuwa moja ya klabu kubwa barani Africa.

Maamuzi hayo yameanza baada ya mchezo wa jana dhidi ya Mbeya City yanayompa Stewart nafasi ya kusaka changamoto mpya sehemu nyingine na kuipa nafasi pia klabu hiyo kuzziba nafasi hiyo.

Klabu hiyo imemshukuru kocha huyo kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa muda wote aliofundisha kwa uweledi mkubwa huku wakiaminini kuwa ataendelea kuwa rafiki wa karibu na shabiki mkubwa wa Azam FC ambaye pia anakaribishwa wakati wowote kwenye klabu hiyo.

Tayari klabu hiyo imeanza mchakato wa mrithi wa Stewart kwa kuzungumza na makocha mbalimbali ikiwa pamoja na kuwafuatilia kwa ukaribu.

Azam FC imemaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu wakati mzunguko wa kwanza wa ligi ulipohitimishwa hapo jana kwa timu hiyo kutoka sare ya kufungana mabaon 3-3.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.